Advertisements

Wednesday, March 29, 2017

TEMESA YAKABIDHIWA BOTI NNE ZA KISASA BAADA YA UJENZI WAKE KUKAMILIKA

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ukodishaji na Huduma za Vivuko TEMESA Mhandisi Japhet Maselle, nyuma yao ni Meneja wa TEMESA mkoani Mwanza Mhandisi Ferdnand Mishamo wakati wa majaribio ya boti Mpya ya MV Mkongo  iliyojengwa kwa ajili ya kutumika katika eneo la Utete Rufiji Mkoani Pwani. Boti hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 40.
 Boti tatu kati ya nne mpya zilizokabidhiwa leo kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Makabidhiano yamefanyikia jijini Mwanza na boti hizo zitasafirishwa kuelekea Pangani Tanga, Kilambo Mtwara na Msangamkuu Mtwara ili zianze kutoa huduma kwa wananchi.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MHE. RAIS DKT. MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam.

Kichupa cha leo Madee - Hela Official Video

REA YAMWONDOA MKANDARASI MZEMBE

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye kipaza sauti) akiwatambulisha wafanyakazi wa Kampuni ya Nakuroi Investment Co. Ltd (waliochuchumaa), ambao watatekeleza Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mkoani Singida.
Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Singida. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Mkwese, wilayani Manyoni.

WAZIRI MWAKYEMBE APOKELEWA OFISINI KWAKE DODOMA


 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante ole Gabriel akiteta jambo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na wakati waziri huyo alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura wakati alipowasili Ofisini kwake Mjini Dodoma.

PICHA ZA MATUKIO ZA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiimba wimbo wa uzalendo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi yake Dodoma Machi 28, 2017.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba wimbo wa uzalendo wakati wa mkutano wao wa mwaka katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Flora Bilauri akitoa neno la utangulizi wakati mkutano wao wa mwaka uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma Machi 28, 2017.

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA TANZANIA NA UGANDA ULIOONGELEA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA HADI TANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam, Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).

Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.

PICHA NA IKULU

WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA, PROF. KABUDI ARIPOTI OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AZINDUA ZOEZI LA UTHAMINI

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Ezekiel Odunga akizungumza na wananchi wa kata ya Farkwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la uthamini mali ili kupisha ujenzi wa bwawa la Farkwa.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma akiongozana na baadhi wa Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Wataalamu wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Uvuvi na umwaguliaji, Wataalamu wa Bonde la Kati na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamezindua zoezi la uthamini wa mali za wananchi wa vijiji viwili vya Mombose na Bubutole watakaohama kupisha mradi mkubwa wa Ujenzi wa bwawa la Farkwa mkoani hapa.

Mradi wa bwawa la Farkwa ni mradi mkubwa ambao huenda ukawa ni mkubwa katika Ujenzi wa mabwawa makubwa kuliko yote barani Afrika. Mradi huu uliasisiwa na baba wa Taifa tangu mwaka 1970 utazinufaisha Wilaya za Bahi, Chemba, Chamwino na Dodoma Manispaa na utegemea kutumia pesa za Tanzania zaidi ya Tilioni 2.

Ujumbe wa Wazi wa Eric Shigongo kwa Diamond Platinumz Wazua Gumzo Mitandaoni

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Mhamasishaji na Mwandishi wa Vitabu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo  amemwandikia ujumbe wa wazi mkali wa Afro Pop Barani Afrika, Diamond Platinumz umezua gumzo mitandaoni ambapo kila shabiki amekua akitoa maoni.
Katika ujumbe huo ambao Shigongo aliandika jana Machi 28 na kueleza kuwa ataendelea tena kuandika sehemu ya pili leo Machi, 29 kupitia Instagram yake, Shigongo ameandika hivi. 
========
MY CONFESSION

Upelelezi kesi ya ugaidi waibua tishio la mgomo

By Zulfa Musa, Mwananchi zmusa@mwananchi.co.tz

Arusha. Washtakiwa wa matukio ya ugaidi ikiwamo urushwaji wa mabomu katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha wametangaza mgomo wa kuhudhuria mahakamani ili kushinikiza kukamilishwa upelelezi wa kesi dhidi yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Nestory Baro washtakiwa hao walidai wamekuwa wakizungushwa kutokana na mashauri dhidi yao kutokamilika hivyo kukaa muda mrefu mahabusu bila kesi ya msingi kusikilizwa.

Washtakiwa hao 61 wanaokabiliwa na mashtaka tofauti katika kesi 15, walidai wamekuwa wakiambiwa upelelezi haujakamilika, lakini wanaamini kinachofanyika ni kunyimwa haki zao za kikatiba.

RC Simiyu amaliza mgogoro wa wanakijiji na wawekezaji

Mkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu, Meatu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya mwekezaji katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao iliyopo wilayani Meatu, na baadhi ya vijiji vinavyounda jumuiya hiyo. Mwekezaji huyo Mwiba Holdings, amekuwa na mgogoro wa mipaka, mkataba wa kumiliki ardhi na uanzishaji wa ranchi na baadhi ya vijiji hivyo kiasi cha kusababisha kuwa na mahusiano mabaya na wananchi ambao wamekuwa wakisusia misaada mbalimbali inayotolewa na mwekezaji huyo.
Hata hivyo, chanzo halisi cha mgogoro huo kimegundulika kuwa ni viongozi wa baadhi ya vijiji ambao wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi huku wakisambaza taarifa za upotoshaji juu ya mwekezaji huyo na kujenga chuki kwa wananchi. Vijiji vinavyounda WMA ya Makao ni pamoja na Makao, Iramba ndogo, Sapa, Mwangudo, Jinamo, Lukale, Mbushi, Mwabagimu na Sunga.

Messi afungiwa mechi nne Argentina

Lionel Messi amefungiwa mechi nne za kimataifa saa tano kabla ya mchezo wao wa jana usiku na Argentina wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Bolivia.

Kiungo huyo mshambuliaji wa Argentina na Barcelona alishushiwa adhabu hiyo kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi wa pembeni wakati wa mchezo wao wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile.

Messi, ambaye alifunga bao pekee katika mchezo huo, alishikwa na hasira wakati mshika kibendera liponyoosha kuashiria kuwa nahodha huyo alicheza rafu, kitendo kilichomfanya amshushie maneno.

Nape: Nitaendelea kuwa mtiifu kwa Rais Magufuli

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema ataendelea kuwa mtiifu kwa Rais John Magufuli, Serikali na Chama cha Mapinduzi tofauti na maneno yanayosemwa mitandaoni.

Tangu alipoachwa kwenye mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Machi 23, kumekuwa na taarifa nyingi feki kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuenguliwa kwake zikidaiwa kutolewa na mbunge huyo wa Mtama ambazo hata hivyo, amekuwa akizikanusha.

Akizungumza jana wakati akikabidhi ofisi kwa waziri mpya wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe katika ofisi za wizara hiyo mjini hapa, bila kutaja maneno hayo ya mitandaoni, Nape alisema ataendelea kumuunga mkono Rais katika dhamira yake njema ya kuleta mageuzi nchini.

WAKURUGENZI NCHINI WACHAGUA VIONGOZI WAO MD KAYOMBO JOHN AWA MUWEKA HAZINA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA wa Wakurugenzi nchini
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi nchini

SHIRIKA LA EfG LAPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA SOKO LA MCHIKICHINI NA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Soko la Ilala Mchikichini, Jumanne Kongogo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kupungua vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya kufanyika kampeni mbalimbali za kupinga ukatili huo zilizofanywa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kwa kipindi cha miaka mitatu.
  Mwenyekiti wa Soko la Kisutu, Taminu Chande, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kupungua vitendo vya ukatili katika soko hilo. Kushoto ni Katibu wa soko hilo, Suitbert Nyawalla.

MTANZANIA ALIYEWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MUDA MFUPI AMUANGUKIA WAZIRI MWAKYEMBE

Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka.
Gaudence Lekule akipanda mlima Kilimanjaro huku akikimbia wakati akiweka rekodi baada ya kutumia muda wa saa 8:36 mapema mwaka huu.

UFAFANUZI WA ACACIA DHIDI YA TUHUMA ZA USAFIRISHAJI WA MAKINIKIA YA DHAHABU/SHABA


Zimepita wiki tatu (3), tangu kutangazwa kwa zuio la ghafla la ushafirishaji wa makinikia ya dhahabu/shaba lililotangazwa tarehe 2 Machi. Tangu kutangazwa kwa zuio hilo kumekua na upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hadi sasa, Acacia haikutoa tamko lolote hadharani, sababu tumekua tukielekeza jitihada katika kutafuta muafaka na Serikali juu ya nini kifanyike. Lakini, kutokana na kiwango kikubwa cha taarifa potofu na zisizo sahihi zenye uvumi mwingi ambao unaweza kutuletea taswira mbaya kwa kampuni, kwa wafanyakazi wetu na pia kwa Tanzania kwa ujumla, tumeamua kuweka wazi hali halisi juu ya hoja mbalimbali.

Acacia inapinga vikali kuhusika na madai yaliyotolewa mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya ukaguzi bandarini – Dar es Salaam kwamba sisi tulikua tukifanya njama za kutorosha makontena yenye makinikia ya dhahabu/shaba nje ya nchi licha ya katazo lililotangazwa na Serikali. Ukweli ni kwamba si Acacia wala wateja wetu walijaribu kusafirisha makinikia haya nje ya nchi.

Kabla ya kutangazwa kwa zuio hilo, makontena, 256 ambayo sasa yamehifadhiwa ZamCargo (zamani ikijulikana kama Mofed - ambaye ni wakala wa usafirishaji wa forodha Customs Freight Services, CFS) yalikuwa tayari yamesafirishwa kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, na makontena mengine 21 yaliyokutwa katika bandari ya Dar es Salaam yakiwa tayari yameidhinishwa na idara ya forodha ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na yalikua tayari kusafirishwa. Zoezi hili huwa linajumuisha TRA pamoja na Wizara ya Nishati na Madini (MEM) ambao kwa pamoja wanahusika katika mchakato wa kusafirisha mikinikia nje ya nchi kwa utaratibu maalum.

MAGAZETI YA LEO MARCH 29, 2017

Tuesday, March 28, 2017

A NIGHT OF EMPOWERMENT AT CRYSTAL LOUNGE

SWAHILI MEDIA INAKULETEA RAHA ZA PWANI FRIDAY MARCH 31, 2017 HAMPTON INN

KARIBUNI KWA IBADA YA JUMAPILI YA TANO YA KWERESMA BISHOP ELIAS CHESSA KUTOKA TANZANIA ATAHUBIRI NENO LA MUNGU

Wana wa Mungu wetu aliye hai, Amani iwe kwenu.Karibuni kwa Ibada ya Jumapili ya tano ya Kwaresma, April 2, 2017. Mtumishi wa Mungu kutoka Tanzania, Bishop Elias Chessa ATAHUBIRI NENO LA MUNGU siku hiyo. Wenye mahitaji mbalimbali  wataombewa.

Anuani yetu ni:

Swahili Lutheran Church (at Living Faith Lutheran Church)
1605 Veirs Mill Rd.
Rockville, MD 20851

Image result for BISHOP ELIAS CHESSA

MTOTO WA MTANZANIA PATRICIA AONGOZA KATIKA SHINDANO LA REGIONAL LEVEL, CHARLOTTE, NC

Patricia Tayn mtoto wa mama Mtanzania anayesoma Blessed  Sacrament Middle School ya Burlington, North Carolina ameibuka mshindi akiwa msichana pekee  kwenye mashindano ya Regional level katika masomo ya Sayansi na hisibati yaliyofanyika Charlotte, North Carolina siku ya Ijumaa March 24, 2017.
Patricia Tayn mwanafunzi wa kwanza kushoto (mwenye fulana ya bluu) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wengine kutoka shule mbalimbali jimbo la North Carolina walioshiriki shindano hilo.
Wapili toka kushoto ni Patricia Tayn akiwa katika picha ya pmoja n familia yake. wakwanza kushoto ni mama yake Scolla Tayn na watatu toka kushoto ni Bwn. Tayn baba ya Patricia.

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI WA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AHADI, ILANI YA CHAMA TAWALA NA MAAGIZO YA VIONGOZI WAKUU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza umuhimu wa mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma na kulia kwake waliokaa niNaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasilisha hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.

Na. Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amezindua mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu ulianzishwa kwa lengo la kusaidia upatikanaji na utoaji wa taarifa za utekelezaji kupitia mfumo wa kisasa (kidigitali).

Akizindua mfumo huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Machi 28, 2017 Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu wa mfumo huo kuwa umejikita katika kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za utekelezaji wa Maagizo yao na yale yaliyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.

“Mfumo huu utasaidia sana katika kufuatilia shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa maazigo yote na ahadi zilizotolewa ili kuona utekelezaji wake kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema Mhe.Waziri.

ALL GOALS: Taifa Stars vs Burundi March 28 2017, Full Time 2-1

LIVE IN DALLAS TEXAS....."MARIMBA AFRIKA BAND"

Get Ready People "Live in Dallas Texas..."Marimba Afrika Band" is coming down to share the fun with you on Tanzania Day!!! Calling all Africans to come out no matter where you are from, we have a song for you!

MSHAURI WA MANDELA AFARIKI DUNIA

Kiongozi mwanaharakati aliyeshiriki sana kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87, wakfu wake umetangaza.
Bw Kathrada alifariki dunia akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg "baada ya kuugua kwa muda mfupi, kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye ubongo wake".
Pamoja na Nelson Mandela, Bw Kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane wa African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 1964.
Walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi.
Bw Kathrada alikaa jela miaka 26, 18 kati ya miaka hiyo akiwa katika gereza hatari la Robben Island.

OLD SCHOOL REUNION, COLUMBUS, OH KUWAKA MOTO LABOR DAY NICO NA RENATUS NJOHOLE KUINGOZA SIMBA UGHAIBUNI, WACHEZAJI WALIOTAMBA PAZI, VIJANA, DON BOSCO KUONYESHANA MAUJUZI

Kikosi cha Simba kikiongozwa na Nico na Renatus Njohole Dallas, Texas.
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba kikiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Wilson Masingingi na mkewe siku walipotwaa ubingwa Dallas, Texas wakati wa kongamano la DICOTA
Kulia ni mkuu wa Wilaya Mhe. Kasesela akiwa Hoston katika picha ya pamoja na wachezaji wa Pazi enzi hizo Vitalis Gunda na Atiki Matata aliyekuja toka Uingereza kuiwakilisha Pazi.
Timu ya Tanzania iliyoundwa na wachezaji waliotamba enzi hizo katika timu za Pazi, Vijana, Don Bosco na kwengineko wakinyanyua juu kikombe walicho kipata baada ya kuifunga timu ya Gabon

NAPE AMKABIDHI RASMI OFISI WAZIRI MWAKYEMBE

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiwakaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitoa neno kwa Waziri mpya na Waziri aliyepita wakati wa makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.

FIFA kumlipa mshahara Coleman kwa kuvunjwa mguu


Shirikisho la soka duniani FIFA limethibitisha kuwa litamlipa mshahara beki wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland na klabu ya Everton Seamus Coleman kwa kipindi chote atakachokuwa anauguza mguu wake.
Coleman alivunjika mguu wake wa kulia ijumaa iliyopita katika mechi dhidi ya Wales baada ya kuchezewa rafu mbaya na beki Neil Taylor, mechi hiyo iliisha kwa sare ya 0-0.

Siku ya jumamosi Coleman alifanikiwa kufanyiwa upasuaji na sasa anataraji kukaa nje ya uwanja kwa muda wa takribani miezi 6 akijiuguza.
FIFA kupitia (Fifa Club Protection Programme) wamethibitisha watakuwa wanamlipa mchezaji huyo kwa kipindi hicho chote atakachokuwa nje ya uwanja. Mshahara wake ambao kwa wiki ni Pauni 50,000.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MGODI WA BUZWAGI NA KUCHUKUA SAMPULI ZA MCHANGA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifanya ziara katika Mgodi wa Buzwagi  27 March 2017 kwa ajili ya kuangalia  Mchanga  uliowekwa katika  Makontena  kwa ajili yakusafirishwa nje ya nchi katikati ni Mkuu wa  Mkoa wa Shinyanga  Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja  Mkuu wa  Mgodi wa Buzwagi Bwana  Stewart Hamilton. Picha na PMO 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Sampuli ya Mchanga wenye Dhahabu unao safirishwa nje ya Nchi na Mgodi wa Buzwagi  uliopo Kahama Mkoani Shinyanga  Waziri Mkuu Alifika katika Mgodi huo tarehe 27 March 2017 kuangalia na kuchukua Sampuli ya Mchanga  ili Serekali ikaupime katika Maabara za Serekali.