Advertisements

Tuesday, December 2, 2014

TRA YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA - KAHAMA

 Baadhi ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na mamlaka ya mapato TRA kahama la shirika la muvuma.
 Hili ndiyo jengo la ushirika la muvuma la kusaidi watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi mjini kahama jengo hili kwa sasa ilinaitajika uzuio kwa ajili ya usalama kwa watoto hao .
 Meneja wa TRA kahama Peter Nkwabi akisalimia na muweka hazina wa shirika la muvuma
 Mjumbe wa shirika la muvuma Eliulie Matina alinyosha mkono kuonyesha baadhi ya maeneo ya jengo la watoto yatima kwa maofisa wa tra alijikuja mikono ni meneja wa tra wilaya ya kahama Peter Nkwabi wakati walipotembelea jengo hilo na kutoa matofari mia mbili ya ujenzi wa uzio.
 Baadhi ya watumishi wa mamlaka ya mapato wilaya ya kahama wakiwa wamembeba baadhi ya vitu mbalimbali vya msaada kwa kituo cha watoto yatima .
 Katibu wa shirika la muvuma Rehema konyonga akisoma Risala kwa mgeni Rasmi meneja wa tra kahama hayupo pichani
 Baadhi ya  wanafunzi  wa kituo cha muvuma mwenye kofia ni Jemes Fransi anasoma kidato cha pili kati ni mabula magandula na mwisho ni Jackielin pius anasoma kidato cha pili  wakiwa angalia wafanyakazi wa TRA wilaya kahama wakati wamefika katika nyumba yao huku nyuma kukiwa na matofari  mia mbili kwa ajili ya ujenzi wa uzio .
 Baadhi ya wajumbe wa muvuma wakiwa na meneja wa TRA mwenye tai wakisikilaza Risala
 Baadhi ya watumishi wa TRA Kahama na shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisilinza Risara ikisomwa na katibu wa kikundi hicho cha muvuma .
 Baadhi ya watumishi wa TRA na wajumbe wa muvuma wakati wa kutoa msaada mbalimbali katika nyumba yao ambayo imefika hatua za mwisho ambapo TRA wametoa matofari mia mbili kwa ajili ya ujenzi wa uzio .
 Watumishi wa TRA Wakitoka nje ya jengo muvuma baada ya kulikangua jengo hilo .
 Baadhi matofari ambayo mammlaka ya mapato imeyatoa katika kituo cha watoto yatima na waoishio katika mazingira hatarishi cha muvuma mjini kahama.
 Katibu wa shirika la muvuma Rehema konyanga akimkabidhi meneja wa mapato kahama Peter Nkwabi Risala ya hotuba yao.
 Mwenye Tai ni meneja wa mamlaka ya mapato TRA Nkwabi Peter kulia ni Zelia kilimba mwenye kitenge bengani .
 Meneja wa TRA Nkwabi Peter akiongea na wanafunzi wa kituo cha muvuma mwenye bahasha ni  Jackieli Pius na mwenye kofia ni Jemes Fransi wakibadilisha mawazo .
 Watumishi wa TRA wakiwa wamebeba vitu mbalimbali kwa ajili ya kutoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima cha muvuma .
 Hapa ndiyo kituo cha muvuma kilichopo kata ya  Nyahanga mjini kahama ambapo watumishi wa TRA walifika hapo kuwasaliamia .
 Karibuni hayo ni maneno ya muweka Hazina wa kituo Zeluia kilimba mwenye kitenge shingoni wakati wamefika kituoni hapo  Nyahanga .
 Kituo cha muvuma Nyahanga wakiwa na wafanyakazi wa TRA wakibadilishana mawanzo kituoni hapo .
 Gari la kumbeba matofari likiwa na matofari na kuweka katika kituo cha muvuma.
 Watoto wa kituo cha yatima cha muvuma wakiwa wamebeba mfuko wa sukari
Baadhi ya wajumbe wa muvuma wakibadilishana mawazo katika viwanja vya ujenzi wa jengo lao.
  /
       Kahama 

Mamlaka ya mapato ya mkoa wa shinyanga (TRA) yatoa msaada kwa watoto yatima na watoto waishio katika mazingira hatarishi cha (muvuma) wilayani kahama.

Aidha meneja wa( TRA ) wilaya ya kahama Peter Nkwabi alisema msaada huu ni vitu mbali mbali  vikiwemo ,mchele,kilo 100,sukari kilo 50,mafuta ya kupikia lita 20,na matofali ya ujenzi wa uzio matofali 200 na kusema vitu vyote vinadhamani ya milioni 2.4.

Meneja  wa wilaya ya kahama Nkwabi alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kunguzwa kwa watoto hao katika kituo hicho cha muvuma ambapo kituo hicho kina watoto 19,watoto hao wanakaa katika nyumba ya mtu binafsi jambo ambalo linawafanya watoto hao kuishi kwa tabu.

Aidha Peter alizidi kusema kuwa hali hii ni yakila moja wetu ambaye amenguswa na jambo hili na pia wajibu wa kila mzazi kuona kutuza watoto wao na kuepusha migongoro ya kifamilia.

Kwa upande wao katibu wa shirika la  muvuma Rehema konyanga akisoma Risala ya kikundi hicho alisema kuwa kikundi hicho kiliazishwa mwaka 2002 na kusajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali (NGO)Mwaka 2005. Kuwa na wanachama jumla 20.

Aidha katibu huyo alizidi kufafanua kuwa shirika hilo liazisha kituo mwaka 2007 kikiwa na watoto 12na kwa sasa wapo watoto 19,na baada ya moja kumalizama mafunzo ya uuguzi ngazi ya cheti na kupangwa kufanya kazi hospital ya sikonge mkoani Tabora .

Rehema alisema kuanzishwa kwa kituo hiki kimekuwa na mafanikio ya kuridhisha kwa kupata huduma za malazi,Afya,Elimuna mavazi ,watoto kupata matumaini ya kusoma na baadaye  kuwa na maisha mazuri na kielimu watoto wanayo maendeleo mazuri na wako katika ngazi mbalimbali.

Akifafanua zaidi katibu wa shirika la muvuma alisema kuna changamoto nyingi zikiwemo upungufu wa fedha  kwa ajili ya kusomesha watoto upungufu wa chakula na ukosefu wa fedha za kujengea uzio ili kuweka watoto katika hali ya usalama .

Kwa upande wa wanafunzi jackieli pius kidato 2 alisema kuwa katika kituo chetu tunawashuku sana mamlaka ya mapato ya wilaya kwa msaada wao huu ni faraja sana kwetu na tunaomba jumuia zingine ziinge za serikali na zisizo za kiserikali kuwa na moyo wa kusaindia watoto yatima na nao ishi katika mazingira magumu.

Mohab Matukio

No comments: