Advertisements

Saturday, October 31, 2015

MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2015 YATANGAZWA



Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt Charles Msonde 


Wahitimu 518, 034 kati ya 763, 602 waliofanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba iliyofanyika nchini kote kuanzia Septemba 2 hadi Septemba 10, mwaka huu wamefaulu mitihani yao, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limesema leo.
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 67.84, asilimia 10.85 zaidi ya ufaulu wa mwaka 2014 ambapo waliofaulu walikuwa asilimia 56.99.
Dkt Msonde amesema, ufaulu katika masomo yote umeongezeka kwa asilimia kati ya 4.61 hadi 17.22 ikilinganishwa na mwaka 2014 huku watahiniwa wakifaulu zaidi somo la Kiswahili (asilimia 77.20) na kufaulu kwa kiwango cha chini katika somo la Kiingereza (asilimia 48.56.
Amesema kati ya watahiniwa wote waliofaulu 264, 130 ni wasichana ambao ni sawa na asilimia 64.60 ya wasichana wote 408, 900 waliotahiniwa huku wavulana wakiwa 253, 904 sawa na asilimia 71.58 ya wavulana 354, 706 waliotahiniwa.

Bofya hapa chini kwenye mikoa kutazama matokeo ya darasa la saba

CHANZO: NECTA

3 comments:

Anonymous said...

Sio dalasa ni darasa

Unknown said...

mim naipongeza serikali kwan bila wenyw kutiria mkazo kw wanafunz kuongez juhudi tusingefkia hap tulipo leo katk ulimwengu mpya axanten.

Unknown said...

naipongez serikali pamoja n juhud zote z walimu katk kufundxha kwan ndiyo wame2fany tuonekane watu.