Advertisements

Tuesday, August 30, 2016

Misa ya kumbukumbu ya Marehemu Mama Judith Nyakyi

Familia ya Bi.Leah Nyakyi inapenda kutoa shukurani za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki kwa msaada wao wa hali na mali wakati wa kipindi kigumu cha kundokewa  na mama yao mpendwa Bi Judith Nyakyi, ambaye aliaga dunia siku ya tarehe 23 mwezi wa sita mwaka huu wa 2016 huko Tanzania.shukrani pia ziwafikie watu wote waliowezesha kufanyika kwa  Misa takatifu ya kumkumbuka mama yao mpendwa iliyofanyika siku ya Jumapili 28, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani
 Bi Sima Kazaura akisoma neno katika misa takatifu ya kumbukumbu ya mama Judith Nyakyi
 Ft.Patrick Maina (kushoto) na Ft. Mateo(kulia) wakiongoza ibada hiyo ya kumbukumbu
 wanafamilia wakiwa wanafuatilia ibada hiyo ya kumbukumbu iliyofanyika jumapili ya tarehe 28 mwezi huu wa agosti 2016

 Bi Khadija Mondwe,mwana familia akisoma wosia wa shangazi yake,  marehemu mama Judith Nyakyi.
 baadhi ya wana DMV wakifuatilia misa hio takatifu
katika picha  Bi Leah Nyakyi akisimama pembeni ya picha ya marehemu mama yake,
 Bi Leah na Wanawe(kushoto)Nicole na Michelle (kulia)
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments: