Advertisements

Thursday, December 8, 2016

ZINGATIENI MAADILI NA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YENU: NAPE

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watumishi wa Wizara yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Wizara  katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Magreth Mtaka akitoa hoja za wafanyakazi katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akipokea hotuba ya wafanyakazi kutoka kwa Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bibi Magreth Mtaka katika kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Baadhi ya wawakilishi wa watumishi wa  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Taasisi zake wakifuatilia kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara yake mara baada ya kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM


Na Raymond Mushumbusi -WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka watendaji na watumishi wa Wizara yake kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameyasema hayo wakati akifungua Baraza la wafanyakazi la Wizara yake na kusisitiza kwa watendaji kuwasimamia watumishi walio chini yao kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma kwa wananchi.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya uongozi na watumishi utasaidia kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo ya Wizara, Taasisi zake na watumishi katika kuleta maendeleo ya Wizara katika kutimiza wajibu wao.

“Nawataka watumishi wazingatie maadili katika kutekeleza wajibu wao na naamini kwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano  tutarudisha maadili ya Utumishi wa Umma na bado taratibu zinaendelea kusimamiwa ipasavyo”asisitiza Mhe Nnauye.

Mhe. Nnauye amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ana mpango wa dhati wa kurujesha maadili katika Utumishi wa Umma na kuhakikisha heshima yake inarudi.

Alieleza kuwa endapo kuna mtumishi yoyote atakayeshindwa kusimamia suala zima la maadili anapoteza utumishi wake.

“ Wananchi ndiyo tunaowatumikia na ndiyo wanaotufanya tuwepo hapa tulipo wanahitaji huduma bora. Kama hatutazingatia suala la maadili ni hakika hatutaweza kuwatumikia vema” alieleza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara hiyo , Prof Elisante Ole Gabriel ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa  kuhakikisha watumishi wanazingatia maadili na suala hili linafanyika kwa vitendo zaidi na sio maneno ili kuendelea kuunga mkono jitihada za  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli za kurudisha maadili katika Utumishi wa Umma.

“Mhe. Waziri nakuahidi mimi pamoja na watendaji wenzangu tutalisimamia suala hili na kulitekeleza kwa vitendo ili turudishe heshima ya utumishi wa Umma kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kurudisha uaminifu kwa wananchi”alisema Prof Gabriel.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Magreth Mtaka amesema kuwa ni jambo muhimu kwa watumishi kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao katiKa eneo la kazi.

“Niwashauri watumishi wenzangu tuzingatie maadili ya Utumishi wa Umma ili turudishe heshima ya utumishi wa umma na tutoe huduma iliyo bora kwa wananchi” alisema Bibi Magreth.

No comments: