Advertisements

Thursday, January 19, 2017

Jengo kubwa laporomoka Iran na kuua wengi

Haki miliki ya pichaEPAImage captionHakuna kilichobaki wakati jengo hilo la ghorofa 17 lilipoporomoka

Wazima moto wengi wanahofiwa kuaga dunia baada ya jengo moja kubwa kwenye mji mkuu wa Iran Tehran, kushika moto na kuporomoka.

Wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la ghorofa 17 kwa saa kadha, kabla ya kuporomoka kwa sekunde chache.

Zaidi ya watu 200 pia nao waliripotiwa kujeruhiwa kwenye mkasa huo.

Kwa Picha: Moto mkubwa watishia Israel

Betri mpya inayoweza kuzima moto

Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran.

Moto huo unaripotiwa kuanza mwendo wa saa 04:30 GMT siku ya Alhamisi, wakati watu hawakuwa bado wameingia.Haki miliki ya pichaEPAImage captionWazima moto walikuwa wamepambana na moto huo kwa saa kadha

Magari kumi ya kuzima moto yalifika eneo hilo na vituo vya runinga viliripoti kuwa wazima moto kadha walikuwa ndani ya jengo wakati liliporomoka.

Kituo kimoja cha runinga cha serikali kilinukuu afisa mmoja akisema kuwa kati ya watu 50 na 100 wanaaminiwa kukwama chini ya vifusi.Haki miliki ya pichaTASNIM NEWS AGENCY/REUTERSImage captionJengo hilo lilikuwa ghorofa la kwanza refu mjini TehranHaki miliki ya pichaAFPImage captionWaokoaji walifanikiwa kuwaokoa baadhi ya wazima motoHaki miliki ya pichaAFPImage captionBaadhi ya wale waliosurika waliangua kilio

BBC

No comments: