Advertisements

Wednesday, March 29, 2017

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MHE. RAIS DKT. MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam.
a
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha  Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

PICHA NA IKULU


1 comment:

Anonymous said...

Gender equality haipo kwenye hivi vyama vya siasa. Wapo wajumbe 31 katika picha hii,lakini akina mama ni 4 tuu. Katika uchaguzi uliopita Wanawake walipiga kura kwa uwingi zaidi ukilinganisha na Wanaume. Male Dominance for how long?