Advertisements

Friday, April 21, 2017

MCHUNGAJI KIZIMBANI KWA KUFOJI PASIPOTI

Idara Uhamiaji mkoa wa Arusha imewapandisha kizimbani watu watano,akiwamo mchungaji wa kanisa la Pentecostal kwa kosa la kufoji hati ya kusafiria.
Akizungumza na wanahabari leo, Ijumaa, Ofisa uhamiaji mkoa wa Arusha,Ally Dady alisema raia hao wawili wenye asili ya Congo, wakiwa pamoja na mtoto wao, wamebainika kuishi nchini kinyume cha sheria na kujaribu kufoji hati ya kusafiria
Pia alisema licha kubainika kuishi kinyume na sheria nchini,wamefanikiwa kuwakamata na kuwapandisha watanzania watatu ambayo walikuwa wakiwasaidia raia hao wakikongo.
Akitaja watuhumiwa wote alisema raia hao wawili Linda Mbaki Diangwe na Glory Mwanza Lubinga walishtakiwa kwa makosa mawili ikiwamo kutoa maelezo yasiyo sahihi ili kufoji hati ya kusafiria.

No comments: