Advertisements

Wednesday, May 24, 2017

BREAKING NEWS: RAIS MAGUFULI AMTAKA WAZIRI PROF. MUHONGO AJIUZULU

Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia madaraka kwa kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena.

Amemtaka waziri huyo kujitathimini na bila kuchukua muda mrefu aachie madaraka kutokana na suala hilo.

Rais Magufuli amesema hayo baada ya kamati iliyokuwa ikichunguza suala la mchanga kwenye makontena kukabidhi ripoti yao.

Kamati hiyo ya wataalamu wa jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na viwango vya ubora.

Akikabidhi ripoti hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Sh829.4 bilioni mpaka 1.439 Trillion kwa makontena yote 277.

"Licha ya uchunguzi uliofanywa kupitia makontena haya, tumegundua uwepo wa aina nyingi zaidi za madini ambayo hayakuwa yakijulikana na haya yamekutwa na thamani ya kati Sh129.5 bilioni mpaka261 bilioni," amesema Profesa Mruma.

1 comment:

Anonymous said...

Hii ni double-standard. Anamtaka ajiuzulu? Kama alimteua, kwa nini asimfukuze mara moja kama alivyomfanyia Nape? Nafasi ya Nape ilikuwa tayari imeishajazwa kabla hata ya yeye kujua kwamba amefukuzwa. Kwa nini huyu ambaye amelitia hasara Taifa kwa mabilioni ya pesa za madini anapewa luxury ya kubembelezwa? Hasara aliyoileta Nape ni ile ya kumkosoa Bashite, kipenzi wa JPM. Lipi ni more serious kati ya haya mawili?