Advertisements

Sunday, May 28, 2017

DC UBUNGO MHE KISARE AAGIZA KUAZNZA MCHAKATO WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KATA YA KIMARA

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori (Kulia), Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017

Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akizungumza na wananchi wa Kata hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kuzungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akiwaongoza wananchi kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
 Hali ya ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza iliyopo katika Mtaa wa Mavurunza Kata ya KImara
Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kukagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo hilo. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam muda mchache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuzungumza na wananchi wa Kata hiyo. Leo Mei 26, 2017
Wananchi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori mara baada ya kuzuru kujionea eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 26, 2017 ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg John Lipesi Kayombo kuanza haraka ujenzi wa Shule ya Sekondari kwa ajili ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam.

Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mvurunza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kujionea hali ya maendeleo ya elimu sambamba na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo na hatimaye kuzitatua.

Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Kimara, Mtendaji Kata ya Kimara, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa sambamba na Baadhi ya Wananchi wa eneo hilo.

Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo linakuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu kutoa maagizo kama hayo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.

Mhe Makori alisema kuwa madarasa anayoagiza yaanze kujengwa yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amewaahidi wananchi hao kujengwa madarasa kwa viwango vya kisasa.

Naye Moses Mzakwe na Deogratius Stephano ambao ni wakazi wa Mtaa wa Mavurunza wameomuomba Mkuu wa Wilaya kutilia mkazo swala la upimaji wa viwanja ili wananchi waweze kumiliki ardhi huku wakimpongeza kwa kuzuru katika eneo hilo kwani ameonyesha uwezo wa kujali wananchi anaowaongoza.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzungumza na wananchi hao Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kutekeleza sera na kuisimamia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 na kuwaomba watanzania wote kwa kauli moja pasina itikadi za vyama kumuunga mkono kwani atakuwa imara na madhubuti zaidi katika utendaji wake iwapo ataungwa mkono na watanzania wote.

Alisema kuwa Rais Magufuli anapaswa kutilia mkazo zaidi kwa kuwawekea kufuli watu waliokuwa wanalihujumu Taifa kwa wizi na ufisadi katika sekta mbalimbali nchini.

Mhe Manota alisema kuwa tayari zimetolewa jumla ya shilingi milioni mia moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Shule hiyo ambapo mara baada ya kukamilika itawarahisishia wanafunzi kupata elimu bora pasina mateso wanayoyapata sasa kutokana na ukosefu wa shule ya serikali ya Sekondari katika Kata nzima ya Kimara.

MWISHO

No comments: