Advertisements

Monday, November 20, 2017

WATAKWIMU WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA UKUSANYAJI WA TAKWIMU BORA

 Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa benki hiyo Bw. Johnson Nyera akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu barani Afrika iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei Bibi. Ruth Minja na Mwakilishi wa Asasi za Kiraia Bw. Stephen Chacha. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa akisisitiza jambo wakati wa hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya, Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa benki hiyo Bw. Johnson Nyera, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid akitoa neno la shukrani  katika hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki hiyo Bw. Johnson Nyera, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bibi. Elizabeth Talbert akizungumza katika hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Afisa Habari Mwandamizi Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Said Ameir ambaye alikuwa mshereheshaji katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika akifafanua baadhi ya mada zilizowasilishwa katika hmaadhimisho hayo leo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa akifafanua jambo wakati wa hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia majadiliano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwl. Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.
 Mwanafuzni wa Kidato cha Tano kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu Bi. Felister Mande akipongezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa baada ya kuwa mshindi wa pili katika shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa hiyo Bw. Johnson Nyera, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid na Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya.
 Mwanafuzni wa Kidato cha Tano kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu Bi. Edda Magesa akipokea zawadi ya shilingi laki tatu kutoka kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Uchumi wa BoT Bw. Johnson Nyera baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".Kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid na Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya.
 Mgeni rasmi wa katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Johnson Nyera akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi washindi wa shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora" wakati wa maadhimisho hayo leo Jijini Dar es Salaam.  Wanafunzi kutoka kushoto ni Edda Magesa (mshindi wa kwanza), Fred Komba (mshindi wa tatu) na Felister Mande (mshindi wa nne).
 Mgeni rasmi wa katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Johnson Nyera akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Shule za Sekondari Kisutu Wasichana na Azania walioshiriki shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora" wakati wa maadhimisho hayo leo Jijini Dar es Salaam.  Wanafunzi kutoka kushoto ni Edda Magesa (mshindi wa kwanza), Fred Komba (mshindi wa tatu) na Felister Mande (mshindi wa nne).(Picha na: Frank Shija - MAELEZO)

No comments: