Advertisements

Sunday, May 20, 2018

Mwongozo wa Tathmini ya Mazingira Kuchochea Ukuaji wa Uchumi

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe. January   Makamba akihutubia  washiriki wa  hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
  Kaimu  Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Esther Makwaia akiwasilisha maelezo kuhusu muongozo wa  tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akiteta jambo na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe. January   Makamba wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo wa tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti   wa  Kamati  Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na  Mazingira Mhe. Sadiq Morad akizungumzia umuhimu wa  mwongozo wa  tathmini ya mazingira  kimkakati   Jijini Dodoma.
 Kaimu  Mkurugenzi  Mkuu  wa  Baraza La Taifa la Mazingira  Dkt. Vedast   Makota  akizungumza wakati wa  uzinduzi wa  mwongozo wa  tathmini ya mazingira  kimkakati   Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe. January   Makamba  akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla ya  mwongozo wa  tathmini ya Mazingira  Kimkakati Jijini Dodoma.
( Picha zote na Frank Mvungi, MAELEZO)

Frank Mvungi- MAELEZO
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amezindua Muongozo wa Tathmini ya Mazingira  (SEA) ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kulinda mazingira ili yaweze kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta  maendeleo  endelevu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo  Jijini Dodoma Waziri Makamba amesema kuwa dhamira ya Serikli ni kuhakikisha kuwa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Serikali pamoja na wawekezaji inafanyiwa tathmini hiyo ili kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.

"Nawapongeza WWF kwa kazi nzuri za tafiti wanazofanya na hata kupatikana kwa muongozo huu ni matokeo ya kazi nzuri waliyofanya kama wadau wetu ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu kuunga mkono juhudi za Serikali kulinda mazingira " Alisisitiza  Mhe. Makamba

Akifafanua amesema kuwa anazikumbusha Wizara ,  Taasisi na wadau wote wanaotaka kutekeleza  miradi ya maendeelo kuhakikisha kuwa wanazingatia muongozo huo ambao umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inajenga uchumi wa viwanda.

Aliongeza kuwa Ofisi yake ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa SEA  katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hata hivyo alibainisha kuwa ripoti 14 zimeshapata kibali cha Tathmini ya athari za mazingira na kuongeza kuwa changamoto ambayo Serikali  inachukua kwa uzito kwa sasa ni upatikanaji wa Maafisa Mazingira katika Halmashauri zote hapa nchini.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa  kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,  Biashara na Mazingira Mhe. Sadiq Morad amesema kuwa ili Taifa lifanikiwe katika ujenzi wa uchumi wa viwanda unaotegemea zaidi hifadhi ya mazingira hivyo kuwepo kwa muongozo huo ni jambo la kimapinduzi katika sekta ya mazingira.

Aliongeza kuwa Kamati hiyo imeridhishwa na hatua hiyo kwani itasaidia katika kuchochea maendeleo na kukuza uchumi kwa maslahi ya Taifa.


Uzinduzi wa Muongozo huo umefanyika  Jijini Dodoma  na utakuwa chachu ya utunzaji  wa mazingira hapa nchini .

1 comment:

Anonymous said...

HUYU BRO MAKAMBA MBONA HASIKIKI NISINGE IONE HII HABARI NISINGEJUA KAMA YUMO KWENYE SERIKALI YETU.DUU AISEEE.MBONI MAMBO